Prof. Alexander Nyangero Songorwa Mkurugenzi wa Wanyamapori. Prof.Jafari Ramadhani Kideghesho, Mkurugenzi Msaidizi, Matumizi Endelevu ya Wanyamapori Profesa Alexander Nyangero Songorwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori (Wildlife Division ) kuziba nafasi iliyokuwa wazi. Kabla ya kuteuliwa Profesa Nyangoro alikuwa Profesa Mshiriki katika Usimamizi wa Wanyamapori, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro. Pia ndiye aliyekuwa Mkuu wa Idara hiyo ya Usimamizi wa Wanyamapori SUA. Wakati huohuo, Profesa Jafari Ramadhani Kideghesho ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi, kuiongoza Sehemu ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori (Sustainable Utilisation of Wildlife Section). Kabla ya uteuzi huo Profesa Ramadhani alikuwa Profesa Mshiriki katika Usimamizi wa Wanyamapori katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro. Uteuzi huo umetekelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Maimuna Tarishi k...
Comments
Post a Comment