Wednesday, January 9, 2013

Maendeleo ya Lady JayDee na Gadner mlimani Kilimanjaro


Kwa Mashabiki wote wa Lady Jaydee
Lady Jaydee na Gadner pamoja na Cameraman wao Justin Bayo wanaendelea vizuri huko Kilimanjaro, iliwachukua takribani masaa saba kufika kituo cha Horombo hut kilichopo mita3720 wakitokea kituo cha Mandara hut ambacho kipo mita 2700
Siku ya leo ni siku ya kuruhusu mwili kuendana na hali ya hewa(acclimatization day) kwa sababu wapo juu sana toka usawa wa bahari hivyo watatembea kidogo kwenda juu na kurudi tena Horombo ambapo kesho wataelekea kituo cha Kibo Hut kabla ya kuanza kuelekea kileleni siku inayofuata
Tutaendelea kuwahabarisha zaidi kadri guides wetu wanavyotupa taarifa
Asanteni sana
Nawakilisha
-Kilidove Tours

1 comment: